Kuhusu

  1. Historia ya AFARS

AFARS ni shirika lisilo la kiserikali lililobuniwa mnamo mwaka wa 2020 na wanaharakati waafrika, na washika dau wa jamii Helsinki. AFARS ulitokana na maandamano makubwa ya ‘Black Lives Matter’ yalizuka ulimwenguni kote mwaka 2020. Tulipewa msukumo na kuitikia mwito wa hukua hatua baada ya kifo cha kutisha cha George Floyd na pia mwongezeko wa kesi za polisi kutumia nguvu dhidi ya Waafrika watu na wa watu wa asili ya Kiafrika. Shirika hili liliundwa hapo awali haswa kupanga maandamano haya katika kituo cha polisi cha Helsinki.

Sauti ya waafrika na watu wenye asili ya Kiafrika nchini Finland inahitajika kwenye ukumbi wa mazungumzo na majadiliano kuhusu ubaguzi wa rangi nchini Finland. Ingawa kuna uongezeko wa idadi jamii na vikundi vyenye vya asili ya Kiafrika, waafrika hawahusishwi katika mijadala hii. Tunaamini kwamba uongezekaji wa majukwaa na sauti dhidi ya ubaguzi wa rangi zitasaidia waathiriwa kukabiliana na shida hili na hata kusababisha kutokomezwa kabisa kwa ubaguzi wa rangi. Nchini Finland, Waafrika na watu wenye asili ya afrika, wakumbana na ubaguzi wa rangi unaoendelezwa na watu wengine wa rangi.

Katika majukwaa mengi ya majadiliano kuhusu ubaguzi wa rangi, mara nyingi Waafrika hutengwa na vikundi hivyo vinavyoongozwa na watu wa rangi kwa sababu ya ubaguzi wao dhidi ya Waafrika weusi. Tunaelewa na kuheshimu mitazamo yao kuhusu ubaguzi wa rangi, lakini majadiliano haya si ya kujumuisha wote. Ukweli ni kwamba watu wenye ngozi nyeusi na wenye asili na tamaduni tofauti  wana uwezekano mkubwa wa kubaguliwa. Mwafrika mweusi kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara ndiye anayetishiwa zaidi katika mazingira ya kibaguzi. Jamii inapomkubali mwafrika mweusi, itawafaidi pia watu wengine wa rangi ambao watakubalika vivyo hivyo. Hofu ni jukwaa kwa Waafrika wote na watu wa asili ya Kiafrika kushiriki maoni yao kuhusu  ubaguzi wa rangi nchini Finland. Ni wakati muafaka kwa Waafrika nchini humu kusimulia hadithi yao wenyewe na kuchangia katika mazungumzo kuhusu ubaguzi wa rangi nchini Finland.