Dhumuni / Malengo

(a) Kusudi kuu la shirika hili ni kupanga na kuwaleta watu waafrika wote na watu wenye asili ya kiafrika nchini Finland pamoja ili kujinasua, kujiwezesha na kupigania haki za jamii, haki za kibinaadamu, kupinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa kitaasisi tunaokumbana nao Finland.

(b) Kuleta mshikamano miongomi mwa watu wenye asili ya kiafrika.

(c) Kuwakilisha na kuhakikisha jamii inayozingatia usawa ili kupata maisha bora kwa waafrikana  na watu wa asili ya kiafrika Finland.

(d) Kushirikiana na mikakati inayounga mkono kupigania haki za jamii, haki za kibinadamu na kupinga ubagiuzi wa rangi Finland

(e) Kuchochea au kuunga mkono muingiliano na kushiriki kwa jamii yetu katika siasa Finland.

(f) Kumaliza aina zote za ukoloni, uoga wa waafrika na weusi Finland.

(g) Kuendeleza haki za kibinadamu, haki za jamii, usawa na uzingatiaji wa sheria.

(h) Kutetea uwazi, uwajibikaji wa polisi na watekelezaji wa sheria dhidi ya matumizi ya nguvu kwa waafrika na watu wenye asili ya kiafrika Finland

(i) Kuendeleza, umoja, amani na utulivu katika jamii yetu

(j) Kuleta mshikamano na rasilimali kwa waafrika na watu wenye asili ya afrika wanaokumbana na ubaguzi wa rangi ni kupata usaidizi wa kihisia na kiakiliili kushughulikia majeraha na maumuvu yanayotokana na ubaguzi wa rangi na kuwawezesha kuripoti visa hivyo kwa polisi.