Kazi zetu

Tunaelimisha, kuwakilisha na kuchukua hatua – Kupinga ubaguzi wa rangi unaendelelezwa na taasisi na miundo chini Finland. Kwa Pamoja tutaijenga jamii bora ambayo haizingatii tofauti za kikabila, jinsia na migawano ya kidini.

Sisi waafrika na watu wa asili ya kiafrika tunaoishi Finland, tunatambua umuhimu wa kuchukua hatua zifaazo kwa pamoja,  kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd. Kuna umuhimu mkubwa wa kuchukua hatua kwa pamoja ili kuendeleza umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa waafrika wanaoishi Finland. Tunatekeleza haki zetu kubaini hatima yetu, kufuatilia haki zetu za kuwa na uhuru, amani usawa, haki na heshima. Tunafahamu jukumu letu la kuunganisha rasilimali asili na zile za kibinadamu za watu wetu wote nchini Finland na ughaibuni. Tukichochewa na haki zetu za kimsingi za kibinadamu, heshima na kutimiza malengo ya kibinafsi, Tumeridhika na azma ya pamoja ya kuendeleza uelewano na ushirikiano baina ya watu wetu katika jamii. Tumejitolea kuchochea Waafrika wote  na watu wenye asili ya kiafrika Finland, bila kubagua umri, rangi, imani, jinsia, na kabila, ili kuafikia umoja.

Tunatambua hitaji la mchakato unaoendeshwa na watu kuijenga jamii iliyo bora, yenye haki na usawa kwa wote nchini Finland.